SOMO: SASA NAITAKA NYOTA YANGU - ASKOFU GWAJIMA

No Comments

SOMO: SASA NAITAKA NYOTA YANGUMATHAYO 2:1-12
“Yesu alipozaliwa katika Bethlehemu ya Uyahudi zamani za mfalme Herode, tazama, mamajusi wa mashariki walifika Yerusalemu, wakisema,Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? Kwa maana tuliiona nyota yake mashariki, nasi tumekuja kumsujudia. Basi mfalme Herode aliposikia hayo, alifadhaika, na Yerusalemu pia pamoja naye.Akakusanya wakuu wa makuhani wote na waandishi wa watu, akatafuta habari kwao, Kristo azaliwa wapi? Nao wakamwambia, Katika Bethlehemu ya Uyahudi; kwa maana ndivyo ilivyoandikwa na nabii,Nawe Bethlehemu, katika nchi ya Yuda, Hu mdogo kamwe katika majumbe wa Yuda; Kwa kuwa kwako atatoka mtawala Atakayewachunga watu wangu Israeli.Kisha Herode akawaita wale mamajusi faraghani, akapata kwao hakika ya muda tangu ilipoonekana ile nyota.Akawapeleka Bethlehemu, akasema, Shikeni njia, mkaulize sana mambo ya mtoto; na mkiisha kumwona, nileteeni habari, ili mimi nami niende nimsujudie.Nao waliposikia maneno ya mfalme, walishika njia; na tazama, ile nyota waliyoiona mashariki ikawatangulia, hata ikaenda ikasimama juu ya mahali alipokuwapo mtoto.Nao walipoiona ile nyota, walifurahi furaha kubwa mno.Wakaingia nyumbani, wakamwona mtoto pamoja na Mariamu mamaye, wakaanguka wakamsujudia; nao walipokwisha kufungua hazina zao, wakamtolea tunu; dhahabu na uvumba na manemane.Nao wakiisha kuonywa na Mungu katika ndoto wasimrudie Herode, wakaenda zao kwao kwa njia nyingine.

Hawa mamajusi wa mashariki walikuwa ni wachawi au wataalamu wa nyota, kwenye Biblia ya kiingereza wameandikwa Magicians kwa maana ya wachawi, magicians kwa maana ya waganga au astrologers kwa maana ya wasoma nyota. Kipindi hicho kulikua hakuna chombo cha kusomea nyota. Yesu alizaliwa mashariki ya kati na hawa mamajusi walikuwa wakikaa mashariki ya mbali ambapo kutokea huko hadi mashariki ya kati ni masaa saba mpaka nane. Hawa wachawi waliiona nyota ya Yesu wakaanza kuifuata na walikuwa wanasafiri kwa upepo kwa vyombo vya baharihi. Walitokea mashariki ya mbali mwaka mmoja kabla ya Yesu hajazaliwa na kutokana na ushahidi huo tunajifunza kwamba nyota ya mtu inaweza kuonekana na kufuatwa.
Kuna nyota zingine haziwezi kuonekana na nyingine hazionekani, nyota ya mtu isipoonekana elimu yake haionekani, kazi yake haionekani, ndoa yake haionekani. Nyota yako inaweza kufuatwa kwa uzuri au kwa ubaya. Nyota ya mtu inaweza kufuatwa na watu wakatoa manemane na dhahabu.

Nyota ya mtu inaweza kuonekana na mtu huyo akaonekana anapendwa na watu anatafutwa na watu na baada ya muda fulani kupita mtu huyo anaanza kupoteza umaarufu wake,Nyota ya Yesu ilipoonekana mfalme Herode alisikitika sana na watu wake. Kuna wakati nyota ya mtu inapoonekana wafalme wa nchi husikitika kwasababu nyota inakuwa imeonekana. Lazima ujue kwamba nyota ya mtu inapoonekana kuna baadhi ya wafalme hufadhahika kwasababu wao ndio waliokuwa wamezifunika na sasa nyota zao zimefunikwa.Mfalme Herode aliamua kutaka kumuua Yesu kwa siri kwababu alipata hakika ya muda tangu nyota ya Yesu ilipoonekana na alitumia mbinu ya kutaka kwenda kumsujudia kumbe lengo lake lilikuwa ni kumuua Yesu
Nyota yako inapoonekana watajaribu kukuua kwasababu wewe unakuwa umekaa sawa. Biblia inasema wale mamajusi waliendelea kuifuata nyota ya Yesu mpaka ikaeda kutua kwenye nyumba alimokuwemo. Ina maana nyota ya mtu inapoonekana baadhi ya wachawi wanaweza kukufata mpaka mahali ulipo na wakaitumia. Neno la Mungu huhubiriwa kwa kumleta mtu kwenye maisha ya kila siku.

EZEKIELI 12:13-18
“Naye mkuu aliye kati yao atachukua begani katika giza; naye atatoka kwenda zake; watatoboa mahali ukutani, wapate kuvichukua vyombo vyao nje; atafunika uso wake, kwa sababu hataiona nchi kwa macho yake.Tena wavu wangu nitautandika juu yake, naye atanaswa kwa mtego wangu; nami nitampeleka Babeli, mpaka nchi ya Wakaldayo; lakini hataiona, angawa atakufa huko.Nami nitawatawanya kwa pepo zote wote wamzungukao ili wamsaidie, na vikosi vyake vyote; nami nitaufuta upanga nyuma yao.Nao watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana; nitakapowatawanya kati ya mataifa, na kuwatupa-tupa katika nchi zote.Lakini nitawasaza watu wachache miongoni mwao na kuwaokoa na upanga, na njaa, na tauni ili watangaze habari ya machukizo yao yote, kati ya mataifa huko waendako; nao watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana.Tena neno la Bwana likanijia, kusema,Mwanadamu, ule chakula chako kwa matetemo, ukanywe maji yako kwa kutetemeka na kwa kuyatunza sana”

Wachawi wapo na wameongelewa kwenye Biblia. Kuna watu wamewindwa na Mungu anataka kuwaachilia. Wachawi wapo, hirizi zipo uchawi upo. Na watu wanaweza kuwindwa kama ndege

NAHUM3:4
“Kwa sababu ya wingi wa ukahaba wa yule kahaba mzuri, yule bibi wa mambo ya uchawi, auzaye mataifa kwa ukahaba wake, na jamaa za watu kwa uchawi wake.

ASILI YETU

Mwanadamu ana vipande vikubwa vitatu ambavyo ni Roho ya mtu, Nafsi ya mtu na mwili wa mtu. Roho ilitoka mbinguni “kwa maana Mungu akamfanya mtu kutoka kwenye vumbi, akampulizia pumzi ya uhai ambayo ni roho mtu akatokea. Roho ya mtu inatoka kwa Mungu.

WAEBRANIA 12:19
“Na pamoja na hayo tulikuwa na baba zetu wa mwili walioturudi, nasi tukawastahi; basi si afadhali sana kujitia chini ya Baba wa roho zetu na kuishi?”

Mungu anaitwa Baba wa Roho zetu, mtu ana baba wa mwili alyezaa mwili na Baba wa Rohoni aliyezaa Roho.

MATHAYO 1:1-5
“Kitabu cha ukoo wa Yesu Kristo, mwana wa Daudi, mwana wa Ibrahimu.Ibrahimu alimzaa Isaka; Isaka akamzaa Yakobo; Yakobo akamzaa Yuda na ndugu zake;Yuda akamzaa Peresi na Zera kwa Tamari; Peresi akamzaa Esromu; Esromu akamzaa Aramu;Aramu akamzaa Aminadabu; Aminadabu akamzaa Nashoni; Nashoni akamzaa Salmoni;Salmoni akamzaa Boazi kwa Rahabu; Boazi akamzaa Obedi kwa Ruthu; Obedi akamzaa Yese”
Kwenye Biblia inaonyesha mwanaume anazaa. Neno kuzaa kwa kiebrania maana yake ni kuleta au kuweka au kuanzisha. Kile kitendo kuziweka mbegu ndani ya tumbo la mwanamke hicho kitendo kinaitwa kuzaa na kile kitendo cha mwanamke kuleta mtoto kutoka tumboni kuja duniani kinaitwa kuzaa kwahiyo mwanamke ana zaa na mwanaume ana zaa.

LUKA 2:6-7
“Ikawa, katika kukaa huko, siku zake za kuzaa zikatimia,akamzaa mwanawe, kifungua mimba, akamvika nguo za kitoto, akamlaza katika hori ya kulia ng'ombe, kwa sababu hawakupata nafasi katika nyumba ya wageni.”

Unaposema umezaliwa na Mungu maana yake umeletwa duniani na Mungu. Baba na mama wanapokutana kimwili maana yake Baba anazaa mwili na Mungu anapoona kitendo hicho kimetokea anachukua Roho anaiweka kwenye tumbo la mama. Maana yake Roho yako ambayo ndio wewe imetoka mbinguni imewekwa na Mungu imezaliwa na Mungu.

ZABURI 2:7
“Nitaihubiri amri; Bwana aliniambia, Ndiwe mwanangu, Mimi leo nimekuzaa.”

Mwanaume na mwanamke wanapokutana Mungu anaangalia kwenye ghala lake anamchukua mtu na kumweka kwenye nyumba yake kusubiria miezi tisa. Tukifika mbinguni sote tunafahamiana kutakuwa hakuna cha mkware, mnyakyusa au mzungu au mchina sababu sote tu wa Baba mmoja.Nyumba ya nje ambayo ni mwili inatengenezwa

1YOHANA 3:7
“Watoto wadogo, mtu na asiwadanganye; atendaye haki yuna haki, kama yeye alivyo na haki;atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi.”
Mungu huangalia duniani na kuangalia tumbo lenye mwili hata kama ni la mwendawazimu, hata kama ni la nje ya ndoa Mungu anaweka Roho yenye kusudi la kufanya hapa duniani kulingana na dunia ilivyo. Kuna wengine wanawekwa kwenye matumbo ya mama wakiwa kijijini lakini kusudi lao ni kuja kuwa wakuu wa nchi.

WARUMI 8:16
“Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu;na kama tu watoto, basi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye.”
Sisi tu watoto wa Mungu na imeandikwa yeye ni kaka yetu mkubwa.Tangu unapotoka mbinguni Mungu anakuwa ameshajua asili yako na kukubariki.

WARUMI 8:29-30
“Maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi.Na wale aliowachagua tangu asili, hao akawaita; na wale aliowaita, hao akawahesabia haki; na wale aliowahesabia haki, hao akawatukuza.” Warumi
Mungu anapouleta duniani ile bidi na ule moyo wa kukufanya utimize ile asili yako anakuwa ameuweka ndani yako. Unapokuja duniani na kuingia ndani ya tumbo la mama yako unakuwa umeshajazwa unachotakiwa kufanya.

YEREMIA 1:5
“Maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi.”

NYOTA NI NINI?
Ni ule uwezo na potential unazotakiwa kufanya. Mwanasiasa haanzi kwasababu ya kufanya siasa mwanasiasa anaanza kwasababu ametoka mbinguni akiwa mwanasaiasa.

ISAYA 47:13
“Umechoka kwa wingi wa mashauri yako; basi, na wasimame hao wajuao falaki, wazitazamao nyota, watabirio kila mwezi mambo ya mwezi huo, wakakuokoe na mambo yatakayokupata.”

Farack maana yake ni elimu ya uganga, kuna watu wanaitwa wazitazamao nyota ambazo sio hizi za angani. Mtoto anaposhuka kutoka mbinguni mpaka kwenye tumbo la mama yake akiwa ananyota ya uwaziri au uraisi au akili au ufahamu au biashara. Wasoma nyota hao wanaamua kuifuata nyota mpaka mahali ilipofikia kwa mtoto aliyenayo na anaweza akawa amezaliwa au hajazaliwa.

Shetani ni mwizi hana uwezo wa kujenga au kuanzisha kitu ni mwizi. Watu washirikina wanaotaka kupata madaraka ya uongozi au kuwa wafanya biashara wanaamua kwenda kwa waganga wa kienyeji na mganga anapomwangalia mtu huyo anamwona hana kitu na kumwambia njoo kesho. Mganga huyo wa kienyeji anaposema njoo kesho anakuwa anaamua kuingia kwenye ulimwengu wa rohoni na kuangalia nyota ya utawala au biashara au ndoa na kuiona kwa mtoto Fulani mahali popote na anaamua kwenda kuifuata na kuichukua.watu wanaposema shetani ni mwizi maana yake anaiba nyota za watu kupitia mawakala wake kwa stahili hiyo.

Nyota hizo zinaweza kuwa za kuzungumza au mvuto au ujasiri na mwanasiasa Fulani anayetaka nyota anaendaka kuchukua nyota hizo kwa mganga wa kienyeji na kuzipata kwa stahili hii. Mwanasiasa huyu anakuwa amejaza nyota za watu na mafanikio yake yanatokana na watu aliowaibia nyota unakuta mwanasiasa huyu amefanikiwa kupendwa na watu, kibali, kuongea, ujasiri sababu nyota alizoziiba zinakuwa zinafanya kazi hiyo.
Mahali ambapo unapata taabu ndipo ambapo nyota yako ilipo, mafanikio yako halipo. Unaweka ukawa unamchumbia mtu akakuangalia na kukutukana sababu umeibiwa nyota yako ya usoni, msichana anaweza akawa anachumbiwa na wazee sababu anaonekana mzee na nyota yake ya urembo imeibiwa.
Kuna wengine wanakuwa wanatumia nyota za watu bila ya wao kujua sababu walikwenda kwa waganga wa kienyeji kutaka mafanikio wakapewa nyota za watu na hao lazima nyota hizo ziondoke kwao kwa jina la Yesu.

Kila unachotaka kuwa nacho ufanikiwe tayari unacho ili uwe ambavyo Mungu anataka uwe. Unaweza kuwa umesharudisha nyota yako tayari lakini hujui kama unayo unatakiwa uhame kwenye ulimwengu wa rohoni uingie kwenye ulimwengu wa mwilini ili ungae kama unavyotakiwa kuwa.

MTU AMBAYE NYOTA YAKE IMECHUKULIWA NA WATU ANAONEKANAJE.

Unaweza kumkuta mtu Fulani maarufu sana anakupenda unamwota kwenye ndoto unakuwa unaota unamsaidia kazi zake, unaota umekuwa unongea naye, ndoto ni kiashiria cha kitu kin achokuja kutokea baadaye kweynye maisha yako, ukigundua hivi anza kufanya vita mahali hapo kwa kumpiga na kushambulia huku ukiita nyota yako irudi kwa jina la Yesu.

Watu wengine wanaugua kwasababu kuna mtu ana nyota zao anazitumia na anajua ipo siku nyota itarudi na wao wamekuwa mawaziri matajiri, wamesafiri, wametawala lakini hutakiwi upnye magonjwa bali unatakiwa uzudishe nyota yako na magonjwa yataondoka yenyewe kwa jina la Yesu.

Kwa kawaida nyota ya mtu inaporudi inarudi na ule utajiri unarudi na akili inarudi na mchumba anakuja na uwaziri unakuja, na safari zinakuja na ubunifu unarudi kwa jina la Yesu. Unaposema nyota ya uso inamaanisha nyota ya upendeleoa wa uso ulio ndani ya mtu, kuna vitu mtu anavipata shuleni na vingine anavipata kutoka kwa Mungu vilevvile alivyo.

Wakati mwingine mtu aliyeibiwa nyota anapumbazwa na mashetani anakuwa mtu wa kuamka asubuhi na kunywa supu, kusoma magazeti na kupiga stori vijiweni bila kuhangaika nyota irudi sababu ya kupumbazwa.

Tunatakiwa tuwanyanganye waliomiliki kwasababu ya nyota zetu wafilisike na nyota zetu zirudi kwa jina la yesu kristo

UKIRI

Nyota njooo kwa jina la Yesu, nyota ya biashara, nyota ya kazi, nyota ya kusafiri nilitoka mbinguni na mbingu inanijua mimi ni mfanya biashara, wanajua mimi ni tajiri wanajua mimi nikisema kitu kunakuwa vilevile na mimi nimegundua nyota yangu haipo na sasa nataka nyota yangu kwa jina la Yesu.
Mtu aliyechukua nyota yako ukiirudisha atakuchukia vibaya sana sababu atahisi umemwaribia mambo yake.
Nyota yako ikionekana kazi zitakutafuta zenyewe, zawadi zitakufuata mpaka ulipo, promotion zitakufuata popote ulipo kwa jina la Yesu.

Unapoanza kunyanganya aliyekuibia nyota yako utaanza kuona mipango ya kuanza biashara, kutafuta kazi, kusafiriinaanza kuja na ukiona hivyo ujue nyota yako imerudi na uanze kuchukua hatua ya kufanya biashara, kutafuta kazi na utaanza kufanikiwa sababu nyota yako imerudi.

Marko 6:7
“Akawaita wale Thenashara, akaanza kuwatuma wawili wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafu”

MAOMBI
Ninaamuru kwa jina la Yesu mwanasiasa yeyote aliye na nyota yangu ninamnyanganya kwa jina la Yesu, mfanya biashara aliye na nyota yangu namnyanganaya kwa jina la Yesu, mfanya kazi yeyote aliye na nyota yangu namnyanganaya kwa jina la Yesu. Naamuru nyota yangu njoo kwa jina la yesu. Nabomoa madhabahu za kafara ya damu inayonena kushikilia nyota yangu kwa jina la Yesu, ninabomoa madhabahu za kichawi kwa jina la Yesu.

Dear readers, after reading the Content please ask for advice and to provide constructive feedback Please Write Relevant Comment with Polite Language.Your comments inspired me to continue blogging. Your opinion much more valuable to me. Thank you.

0

Post a Comment